1. Tarehe10 Desemba, 2019, Burundi itajiungana na nchi zingine za dunia katika maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 71 ya Tamko juu ya Haki za Binadamu Ulimwenguni kote ili kusisitiza tena jinsi nchi hizo zilijitolea kwa lengo ya kukuza na kulinda haki za binadamu.

2. Tamko hili ambalo ni msingi wa uhuru, haki na amani ulimwenguni, ilipitishwa tarehe 10 Desemba 1948 na azimio 217(III) A la Mkutano Mkuu wa wa Umoja wa Mataifa baada ya Vita kuu ya pili. Siku hiyo ni tena kufunga shuguli za kampeni ya Siku 16 ya uharakati dhidi ya unyanyasaji dhidi ya wanawake na wasichana, toleo la 2019.
3. Burundi inaadhimisha siku hii wakati kunalipolia amani na usalama katika mikoa yote ya nchi ya Burundi. Mada ya mwaka huu ni
« VIJANA, AMKENI NA MPIGANIE HAKI ZA BINADAMU KWA KUFANYA KAZI ZA MAENDELEO YA NCHI »
4. Mada hii ilichaguliwa kwa kuzingatia maadhimisho ya miaka 30 ya kuwepo Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Mtoto, na ikajulikana kuwa zaidi ya nusu ya idadi ya watu duniani ni vijana.
5. Hapa kwetu, Sherehe za siku kuu hiyo zitafanyika Ijuma Disemba 13, 2019, katika mji mkuu wa tarafa ya MUGAMBA Mkoani BURURI.
6. Tunatoa mwaliko kwa wananchi wote wa Burundi na wageni pia, hususani wenyeji wa Tarafa ya Mugamba, kushiriki kwa wingi katika sherehe za maadhimisho ya Siku kuu hiyo.
7. Kwa warundi wote, tunawatakieni siku kuu njema, amani, ulinzi na heshima ya haki kwa kila mwanadamu.
Mungu awabarikieni! Asanteni sana.