1. Tarehe mosi Oktoba kila mwaka, dunia inaadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wazee.
2. Mwaka huu mandha ya kimataifa na pia iliyochaguliwa katika nchi yetu ni « Kuadhimisha mabingwa wa haki za wazee. »
3. Katika mazingira ya kuhifadhi jamii, hatua zifuatazo zimechukuliwa na Serikali ya Burundi:
kutiwa saini makubaliano ya kushirikiana na Vituo na Mashirika anaofanya kazi kwa manufaa ya wazee kama kupewa msaada wa kifedha kila mwaka, kulipa bili za maji na umeme na msamaha wa ushuru kwa bidhaa na huduma kutoka nje kwa ajili ya kuasadia wazee; kutembelea na kugawa msaada wa chakula na vifaa mhimu kwa vituo na mashirika hayo, msaada wa matibabu kwa wazee walio katika hali duni; Pensheni na kadi ya Shirika la ku hudhumia kiafya wafanya kazi wa selikari hutolewa kwa wastaafu.
4. Pia, katika mwaka wa 2012, Serikali yetu imepitishwa Sera ya Taifa kwa ajili ya Ulinzi wa Jamii na Mkakati wa utekelezaji wake ni tayari katika mahali pamoja na Mfuko wa Msaada kwa ajili ya Hifadhi ya Jamii « FAPS ». Mkakati huu na mfuko vinatilia manani makundi ya wasiyojiweza kwa ujumla na hasa wazee.
5. Ijulikane kwamba , nchi yetu ina mpango wa maendeleo wa Taifa (2018-2027) ilizinduliwa tarehe 22 Agosti mwaka huu na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya katika mkoa wa Gitega na mapendekezo maalumu ametolewa kwa taasisi zinawapa hudhuma mbalimbali watu wazee .
6. Mbali na utafiti wa upembuzi kwa ajili ya kutoa hudhuma bure ya afya kwa faida ya wazee wote imegharimiwa na Serikali ya Burundi, pia ilipendekeza kwamba taasisi zinazoshughurika na mambo ya ustaafu kutafuta njia ya kuboresha kiwango ca kiinua mgongo . Zaidi ya hayo, Shirika la Brothers ‘BENEYOZEFU « limefanya utafiti juu ya mahitaji ya wazee katika baadhi ya matarafa na tunatarajia kuona matokeo ya hiyi kazi.
7. Licha ya hatua hizi zote zilizopigwa na Serikali, ingali kazi kubwa sababu kuna watu wazee ambao bado wako katika hali mbaya sana na wengine kuwa tu wameondolewa hivi karibuni mitaani. Kwa matatizo yote wazee wanakabiliwa nayo , Serikali ya Burundi ina utashi wa kufanya kila juhudi kulingana na uwezo wake ili ihudhumie wazee. Tuna uhakika kwanba hakuna njia yingine ya kufaulu bila kupitia mfumo wa mshikamano vijijini,mfumo ambayo umezinduliwa Julai mwaka huu.
8. Katika nchi yetu, siku ya kimataifa ya wazee itaadhimishwa tarehe mosi Jumatatu, Oktoba 2018 katika Mkoa wa Gitega, tarafani Giheta ambako itajadiliwa swala kuhusu msaada kwa wazee katika mazingira magumu na pia kufuata matokeo ya utafiti juu ya mahitaji ya wazee uliofanywa na Shirika la Brothers ‘BENEYOZEFU « kwa msaada wa World Solidarity Organization .
9. Tatimaye ,tunachukua hiyi fursa kutoa shukrani za dhati kwa vituo, mashirika na mtu yeyote kwa changia katika kuhifadhi wazee na kukaribisha kila mtu kufanya hivyo na kua mfadhili.
10. Siku kuu njema kwa wazee wote!
IDUMU BURUNDI;
TUSHIRIKIANE KWA KUWAHUDHUMIA WAZEE;
MWENYEZI MUNGU AWABARIKI, ASANTENI !!