27 novembre 2024

KAULI YA WAZIRI WA HAKI ZA BINADAMU, USTAWI WA JAMII NA JINSIA KUHUSU MAADHIMISHO YA KUSHEREHEKEA SIKU YA KIMATAIFA YA WATU WENYE ULEMAVU, 2019

1.     Mnamo Desemba tarehe 3 ya kila mwaka, dunia nzima inadhimisha Siku ya Kimataifa ya Watu Walemavu.

Mheshimiwa Waziri wa Haki za Binadamu, ustawi wa Jamii na Jinsia Bwana Martin NIVYABANDI, Akisoma tangazo hili hapo jana jijini Bujumbura (Picha na Elia HARINDAVYI)

2.     Ili Kukuza na kulinda haki za watu wenye ulemavu, hatua kadhaa zilifanywa na Serikali ya Jamhuri ya Burundi kupitia Wizara ya Haki za Binadamu, Ustawi wa Jamii na Jinsia. Hii ni pamoja na ukarabati na ukarabati wa mwili, utoaji wa vifaa vya uhamaji, mafunzo katika taaluma mbalimbali na utoaji wa vifaa vinavyitajika katika jumuia, msaada mbalia mbali hasa wa shughuli za kujipatia kipato kwa vituo na vyama vya walemavu, uwepo wa shule za majaribio katika muktadha wa elimu-jumuishi, n.k.

3.     Mnamo Machi 26, 2014, Serikali ya Jamhuri ya Burundi, ilitangaza Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Watu wenye Ulemavu na tarehe 10 Januari 2018, ilitangaza rasmi Sheria kuhusu Uendelezaji na Ulinzi wa Haki za watu wenye Ulemavu. Tarehe 19 Juni 2019, Sera ya Kitaifa ya kulinda Haki za watu wenye Ulemavu na Mpango wake wa utekerezaji wa mwaka wa 2020-2024 vilipitishwa na Baraza la Mawaziri.

4.     Hata ingawa hatua nyingi tayari zimechukuliwa kwa niaba ya watu wenye ulemavu, kuna vitu vingi bado vinatakiwa kutenda tuzingatia mahitaji makubwa ya jamii hii ya watu walio katika mazingira hatarishi. Hii ndio sababu, pamoja na siku ya mshikamano wa ndani iliyozinduliwa mwaka jana wa 2018, wadau wote katika kitengo hiki wamealikwa kutekeleza sera hii ya kitaifa na mpango wake wa utekelezaji.

5. Maadhimisho ya siku kuu hii yatafanyika Jumanne, tarehe 3 Desemba 2019 katika uwanja wa mpila Ingoma mkoani Gitega, mji mkuu wa kisiasa wa Burundi, kwa maada ifuatayo: « Kukuza ushiriki wa kijamii kwa watu wenye ulemavu kulingana na uwezo wao: ni hatua mojo kwa wakati »

6.     Tunatoa wito wa mwaaliko kwa wakazi wote wa Burundi, haswa wakazi Mkoa wa Gitega na maeneo ya karibu kushiriki kwa wingi katika sherehe hizi.

7.     Kwa watu wote wenye ulemavu, tunawaambia, Siku kuu nyema! Mungu awubariki, asanteni saana!!

Elie HARINDAVYI

Le Coordonnateur de la Cellule de Communication et d'Information du Ministère des Droits de la Personne Humaines, des Affaires Sociales et du Genre

Voir tous les articles de Elie HARINDAVYI →